Lubao FM | 102.2 Hz

Paris St Germain wafanya mawasiliano na wawakilishi wa mshambuliaji nyota wa liverpool Mohamed Salah

Mabingwa wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain wamefanya mawasiliano na wawakilishi wa mshambualiaji nyota wa Liverpool Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 28, ili kumsajili mchezaji huyo tegemezi pia wa timu ya taifa ya Misri. 

Huku Kocha wa PSG Mauricio Pochettino pia amewasiliana na mshambuliaji nyota wa Tottenham na timu ya taifa ya England Harry Kane mwenye umri wa 27, kuhusu uwezekano wa nyota huyo kuhamia Ufaransa. 

Hayo yakijiriMiamba ya soka nchini Ujerumani klabu ya Bayern Munich itajaribu kumsajili kocha wa Liverpool Jurgen Klopp mwishoni mwa msimu endapo kocha wao Hansi Flick ataenda kuitumikia timu ya Taifa ya Ujerumani. 

By Samson Nyongesa

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE