Mwanamme afariki baada ya kudaiwa kubugia pombe ya chang’aa akiwa na njaa huku familia ya mwendazake ikitoa sarakasi kwa kukwamia mwili wake kwa madai kuwa hawakauwa na hela za upasuaji na mochuari Kakamega.
Wanakijii wakiongozwa na Edgar Masengo wanasema mwendazake Eliud Musonye wa miaka 37 aliyekuwa mkaazi wa mtaa wa Mahiakalo viungani mwa mji wa Kakamega anadaiwa kufariki baada ya kubugia pombe bila ya chakula.
Familia ya mwendazake ikiiongozwa na mamake marehemu Elika Bwonya ilizuia maafisa wa polisi kuubeba mwili huo kwa madai kuwa wamesakamwa na hali ngumu ya kifedha ikizingatiwa wanashughulikia babake marehemu Thomas Bwonya ambaye amelazwa katika hospitali kuu ya Kakamega akiwa hali mahututi kwa muda wa siku mbili zilizopita, Huku maafisa wa polisi wakilazimika kuubeba mwili huo kwa lazima ili kufanyiwa upasuaji.
By Richard Milimu