Hatimaye afisa wa polisi aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mumewe ambaye pia alikuwa polisi usiku wa tarehe 6 mwezi huu mjini Nairobi kutokana na mzozo wa kinyumbani, amezikwa hii leo katika kijiji cha Matsakha eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega.

Pauline Wakasa mwenye umri wa miaka 31 aliuawa na mumewe Hudson Wakisa ambaye pia alijitoa uhai kwa kujipiga risasi baada ya kutekeleza unyama huo.

Wazazi wa afisa huyo, Mulongo Tali na Joyce Mwenje wamesema mauaji ya mwanao ni pigo kubwa kwa familia hiyo ambayo ilikuwa ikimtegemea.

“Yani vile nilienda kuona mtoto yangu, marisasi yenye nilipata wamedunga mtoto yangu  sikuamini na kijana yangu amejidunga pia yeye ako huko.Pauline alikua polite girl,tena alikua guide and counseling  girl.Yani angejaribu hata kukuongelesha kwa simu hata kama uko na hasira aje mtotot yangu angejaribu kukurudisha kwa line tena alikua mtu anapenda maneno ya Mungu.

“imekua challenge kubwa kwasababu amlikua mtot wangu wa kwanza na amekua tegemea, imekua challenge kwa familia  mbili, tuliweza kuongea tukiwa mortoury Nairobi  lakini bado kuna pending issues kidogo na mambo ya watotot wajukuu walikuwa wakuje wazike mama yao lakini wataita waliambia tukongee,waliniahidi watakuja leo but wajaonekana kwa hivyo nangoja tumalize hii shughuli ya matanga ndio tufuatilie hii maneno hii maneno

Maafisa wa polisi waliozungumza kwenye mazishi hayo ambayo yalitekelezwa kwa kuzingatia masharti ya wizara ya afya dhidi ya ugonjwa wa covid 19, walimtaja marehemu kama rafiki mzuri huku wakiwataka wananchi kuboresha mahusiano yao na maafisa wa polisi ambao pia ni wanadamu wenye hisia badala ya kujitenga nao.

“sharing is sharing and when you share you reduce your problems by half, maneno kama haya hayangetupata juzi kama bwana ya Pauline angekua anajua kushare angekua na confidence kwa maisha yake na hayangetupata.”

“We are surfering as police service,police service is not in isolation we spell adversities like anybody else so nataka mchukue police like any other normal human being, we come from societies, we come from families,from villages like vile Pauline ametoka hapa so I willwish to advise kama uko na ndugu askari and you see a certain change of behavior it is good you communicate with respect of the family anaitwa you try to solve the problem at large, hakuna familia haina kinonda,hakuna familia yenye mtu aneza simama aseme we live in a perfect world, there is nothing like that.”

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE