Vijana katika wadi ya Butsotso Mashariki eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega wanaitaka serikali kutumia fedha inazokopa kutoka nje kwa ajili ya corona kuwasaidia vijana kujiinua kimapato

Wakiongea baada ya hafla ya kuchangisha pesa kuendeleza mradi wao katika kanisa la Elukho Church of God misheni ya Ingotse hapo jana, vijana hao kupitia kwa mwenyekiti Abel Ong’ale na Thomas Otipa wamesema vijana wameathirika pakubwa kiuchumi kutokana na janga la corona

Wanaitaka pia serikali kuona kwamba inaweka mikakati bora ya kuwawezesha vijana kuendeleza elimu yao waweze kuinuka kijamii

Ni usemi ambao umesisitizwa na wachungaji wa kanisa hilo wakiongozwa na Irene Odera ambao wanasema vijana kuinuka kiuchumi ni nguzo kwa maendeleo ya kanisa

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE