Jamaa mwenye umri wa makamu anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Lubao kwa tuhuma za wizi wa kuku na mabati katika kijiji cha Shilongo lokesheni ndogo ya Lubao,eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega

Jamaa huyu Zacharia Amusutsu alikamatwa baada ya msako mkali uliofanywa na nyumba kumi wa eneo hilo wakiongozwa na mzee wa mtaa huo Ernest Ikutwa

Hata hivyo mlalamishi wa mali iliyoibwa Patrick Shikono ameelezea alivyopoteza kuku wake na mabati tano aliyokuwa amefunikia na mabati yalitoweka kwa njia tatanishi kabla ya kupokea taarifa zilizopelekea kupatikana kwa mshukiwa huyo aliyekuwa ametorokea mafichoni kwenye mto eneo la duka moja kabla ya kukamatwa kwake

Hata hivyo naye mzee aliyekuwa ameletewa mali hiyo ya wizi Francis Machoni mkaazi wa duka moja ameelezea alivyoletewa mali hiyo ya wizi kabla ya kufanya uchunguzi wake na kutinda kununua mabati yaliyoletwa na jamaa huyo kabla ya kupokea fununu kuwa mabati hayo yalikuwa yakitafutwa kwa semi kuwa mabati hayo yalikuwa yamepotea kwa jamaa aliyemtambua na kumweleza kuwa mshukiwa alikuwa na nia ya kumuuzia mabati hayo na kumtaka mshukiwa huyu kuja kuyachukua mabati hayo mwenyewe na kuyarejesha alikokuwa ametoa kabla ya kukamatwa kwake mshukiwa huyo

Kwa sasa mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Lubao akisubiria kufunguliwa mashtaka ya wizi

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE