Wito umetolewa kwa wakulima kutoka kaunti ya Bungoma ambao huchukua mikopo katika shirika la kutoa mikopo kwa wakulima halmaarufu ( Agricultural Finance Corporation) kulipa mikopo yao kwa wakati ufao.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa afisi ya shirika hilo mjini Bungoma,mkurugenzi wa shirika hilo,George Kubai,amesema kuwa kuna haja ya wakulima kuhakikisha kuwa mikopo wanayokopa wanalipa kwa wakati ufao bila kufuatiliwa huku akisema kuwa serikali haina mpango wowote wa kufutilia mbali madeni waliyonayo .
Kwa upande wake waziri wa kilimo kaunti ya Bungoma,Mathews Makanda,akiwataka wakulima kuekeza zaidi raslimali wanazopata kutoka kwa shirikahilo katika kilimo biashara ,akihoji hiyo ndiyo njia muhimu itakayowawezesha kulipa mikopo yao bila tatizo lolote.
By Hillary Karungani