Wananchi wametakiwa kujitokeza na kushiriki mikutano ya masomo inayohusisha uraia yaani Civic Education ili kuweza kujinufaisha maishani mwao.

Akiongea katika kanisa la marafiki la Shirugu  eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega, afisa mtendaji wa shirika la Afrinov mkoa wa Magharibi Benson Khamasi anasema kuwa madhumni ya kuanda mafunzo hayo ni kwa minajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusiana na umuhimu wa kufanya maamuzi yaliyo bora.

Ni kauli iliyoungwa mkono naye  naibu chifu wa kata ndogo ya Malekha  John Luvonga ambaye pia amewataka wananchi kuyapa kipaumbele mafunzo hayo kwa manufaa yao wenyewe.

Kwa upande wao wakaazi waliohudhuria mafunzo hayo wakiongozwa naye Maximillah Osundwa wameelezea kuridhishwa kwao na mafunzo hayo ambayo wanahoji kuwa yatawafaidi pakubwa maishani mwao.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE