Katibu mkuu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT Wilson Sossion sasa anadai kwamba serikali ina njama ya kudinda kutekeleza mikataba za makubaliano na miungano ya wafanyikazi nchini.
Akiongea mjini Kakamega baada ya kuhudhuria mkutano wa wajumbe wa KNUT tawi hilo, Sossion amesema serikali imekuwa ikilemaza shughuli za miungano za wafanyakazi kwa kuhakikisha hazipati fedha kutoka kwa wananchama wake.
Aidha amesema serikali pia imeanza kufadhili baadhi ya viongozi wa chama cha KNUT na lengo la kumng’atua mamlakani.
By Javan Sajida