Hataua kali za kisheria zitachukulia dhidi ya wamiliki wa maeneo ya burudani watakaopatikana wakienda kinyume na masharti yaliyowekwa na serikali katika kuzuia msambao wa virusi vya corona nchini.

Ni usemi uliyotolewa naye kamanda wa polisi eneo la Kabras Paul Mwendwa ambaye amefichua kuwa baadhi ya wafanyibiashara wa kuuza vileo kwenye maeneo ya burudani wamekuwa wakivunja kanuni za covid 19 na hivyo kuweka wateja wao katika hatari ya kuambukizana virusi hatari vya corona akiahidi kuanzisha msako mkali ili kuwatia mbaroni washukiwa na kuwashtaki kwa mujibu wa sheria.

Kamanda Mwendwa aidha ametoa onyo kali kwa wafanyibiashara wanaouza  pombe haramu kuwa vilevile hawatasazwa na mkono wa sheria.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE