Wakaazi wa lokesheni ndogo ya Shisembe kwenye wadi ya Murhanda eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega wametakiwa kwendelea kutilia mkazo sheria za kudhibiti msambao wa virusi vya covid19

Akizungumza katika hafla ya mazishi ya mama Loice Khatenje mamake shabiki sugu wa kituo hiki Joash Abung’ana naibu chifu wa lokesheni hiyo Mike Shivanda amewataka wakaazi hao kufika afisini mwake na kukusanya kadi zao za huduma 

Shivanda amewataka kuwatunza vyema wanafunzi walio nyumbani ikiwemo wa darasa la nne na wale waliokamilisha mitihani ya darasa la nane akiwataka wazazi kuwapeleka wanafunzi hao shuleni wakati utakapofika

Naye mwaniaji wa kiti cha uwakilishi wadi ya Murhanda Edgar Muhanga akitumia fursa hiyo na kuwarai wakaazi kumchagua kama mwakilishi wao kwenye uchaguzi ujao 2022

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE