Katibu mkuu wa elimu Belio Kipsang amekashifu vikali walimu  wanaofukuza wanafunzi shule kwa kukosa kulipa fedha za chakula cha mchana na madawati.

Kipsang akizungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye shule ya upili ya wasichana ya Moi mjini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu.

Ameongeza kuwa shule haifai kuwalazimu wanafunzi kulipa chakula cha mchana inafaa kuwa kwa hiari yao.

Vile vile amesisitiza suala la wanafunzi waliopachikwa mimba baada ya kuwa na likizo mrefu tangia janga la korona liibuke watakamatwa na kushtakiwa kulingana na sheria ya watoto.

Hayo yanajiri baada ya wazazi kulalamika kuwa kuna baadhi za shule zinafukuza wanafunzi kwa kukosa kulipa chakula cha mchana na madawati.

Story by Sharon Lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE