Spika wa bunge la seneti Keneth Lusaka amesifia mtambo mpya wa kiafya uliyozinduliwa rasmi kwenye hospitali ya kibinafisi ya Royo mjini Malava kaunti ya Kakamega akisema utawasaidia wananchi wengi katika eneo hilo
Akizungumza baada ya kufungua rasmi hospitali ya kibinafsi ya Royo mjini Malava spika Lusaka amewataka wananchi kuchangamkia vifaa hivyo muhimu akisema vitasaidia katika kuimarisha afya zao.
Lusaka aidha amewahakikishia magavana kote nchini kuwa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo zitawafikia kwa wakati unaofaa akiwataka magavana kuyapa kipaumbele maswala muhimu ikiwemo sekta ya afya.
Kwa upande wake seneta wa Kakamega Cleophas Malala ambaye pia aluhudhuria hafla hiyo ameonekana kuwatetea wahudumu wa afya wanaoshiriki mgomo huku akiwasuta magavana nchini kwa madai ya kutumia visivyo fedha zizotengewa maendeleo.
Story by Richard Milimu