Zaidi ya familia 2800 eneobunge la Butere zinakabiliwa na tatizo la funza huku walioathirika zaidi wakiwa watoto wenye umri wa kwenda shule
Hii ni kauli yake msimamizi wa shirika lisilo la kiserikali la Food and Tent linaloongoza kampeni dhidi ya funza eneobunge hilo la Butere Paul Obunde
Akizungumza sokoni Lunza kwenye hafla ya kutoa funza kwa wakaazi Obunde amesema kuwa hili linatatiza pakubwa masomo pamoja na shuguli za kila siku za waathiriwa
Obunde aitha amelalamikia uhaba wa miundomsingi kwenye haswa madarasa kwenye shule eneo hilo kama baadhi ya visababishi vya kuenea kwa funza
Obunde-miundomsingi Kwa upande wake mojawapo wa waasisi wa kampeni hizo Aswani wa Aswani amelaumu ufukara na uongozi mbaya Kama chanzo huku akiahidi kuendeleza kampeni hizo ili kukabili tatizo hilo
Story by James Nandwa