Wazazi wa shule ya Mutoto ilioko eneobunge la Malava kaunti ya Kakamega wanaiomba serikali kuingilia kati na kuwasaidia kutokana na makali ya sheria za shule hiyo wakidai kuwa wamelazimishwa kuchimba vyoo vya shule na kutishiwa kuwafurusha wanao shuleni humo ikiwa hawatatii amri hizo.

Wakizungumza na idhaa hii baada ya kufunga kazi hiyo wazazi hao wakiongozwa na mama Sara Chisutia wamehoji kuwa waliamurishwa kuchimba vyoo hivyo baada ya ilani ya kufunga shule kutolewa na idara inayosimamia maswala ya mazingira.

Bi Sarah alieleza “Tumechimba choo futi ishirini na pia tumetoa shilingi miambili za kununua mabati. Tumegonga kokoto, hii yote tumefanya kwasababu watoto wetu wamekaa nyumbani sana na tunataka wasome. Shule ilikua inafungwa kwa sababu haina vyoo vya watoto kujisaidia”

 Aidha wazazi hao wamehoji kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo  Benard Shabaya amewakera na uongozi wa utikiteta ambao huenda utapelekea wazazi hao kushiriki mgomo.

‘’Mwalimu mkuu anatusumbua sana karibu tunagoma. Nashidwa serikali ya kaunti haiwezi tuchimbia choo tumechoka sana’’

Kulingana na Rose Murwa amesikitia swala hilo na kuiomba serikali kuwasaitia .

“Nasikitika sana tunalipa 1500 na tunashangaa kama hii shule iko kaunti ya Kakamega kenya ama iko nnchi ingine” alisema mama Rose Murwa

Hatua zetu za kumfikia mwalimu mkuu wa shule hiyo  Bernard Shapaya hazikuzaa matunda  baada ya kudinda kujibu madai dhidi yake

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE