Wafanyi biashara wa soko la Kambi-Mwanza lililo katika kaunti ndogo ya Malava kaunti ya Kakamega, wanalilia hali ya soko hilo kuwa hairidhishi kwa upande wa usafi.
Wakiongea kupitia kwa mwenyekiti wao kina mama wanaouza samaki kwenye soko hilo, Hellen Luseno anaelezea jinsi wanavyopitia changamoto zikiwemo usalama wa sehemu ya kuuzia samaki kwamba vibanda vyao huvunjwa na kuwafanya kukosa amani.
“Soko ya kambi wameeka nyumba mingi na vibanda vinavunjwa mara kwa mara. Hatuna ata choo na soko la chakula linafaa kuwa safi” alisema mwenyekiti
Mwenyekiti huyo anaiomba serikali ya kaunti ya Kakamega kupitia kwa gavana Wycliffe Oparanya, kuangalia hali ya soko hilo.
Anasema kwamba ombi lao ni kuhusiana na msimu ujao wa mvua ambao utawatatiza mno kwani mahala pa kujikinga wakiendesha shughuli zao za biashara ni kizungu-mkuti.
“ Naomba serikali ya kaunti kujenga mahali pa kujikinga mvua katika soko ya kambi na pia watujengee vyumba vya kujisaidia.”
Story by Sajida Wycliff