Hali ya taharuki imetanda katika kijiji cha Budonga wadi ya Bunyala Magharibi eneo bunge la Navakholo baada ya mzee mwenye umri  wa miaka 70 kuteketezwa kwa nyumba yake na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo kwa madai ya mzozo wa shamba. 

Kulingana na familia ikiongozwa na mwanawe Barasa Wakhanu marehemu kwa jina Francis Sikuku mwenye umri wa miaka 70 alikumbana na kifo chake cha kikatili baada ya kudaiwa kuwaamrisha kuondoka wale waliokuwa wamekodi vipande vya ardhi kwenye shamba lake.

“Vile nilitoka nnje ilikua saa nne unusu usiku siku ya jumanne tarehe mbili na walikua wamemkatakata kwa kichwa mapua mgongo na nikapiga nduru na watu wakakuja alafu sasa ni wiki moja tu nasasa wamemchomea kwa nyumba tumejaribu kumuokoa lakini hatukufaulu”

Majirani wanaelezea kuwa waliamshwa na nduru za marehemu alipovamiwa na kisha nyumba yake kuteketezwa juma moja tu baada ya kushambuliwa kwa  kukatwakatwa na kuwachwa na majeraha mabaya na watu wasiojulikana.

“Nimekaa na yeeye siku tatu na akanielezea kuwa nimejua huyu mtu na ni shamba ananitafutia”

Wenyeji sasa wanaitaka idara ya usalama kuimarisha usalama eneo hilo kando na kufanya uchunguzi wa haraka na kutiwa mbaroni washukiwa wa maafa haya

“Naomba tu serikali itusaidie kwa sababu ni kama watu wahalifu wamezoea sasa atujui tutalala wapi kwa iwa ama kwa nyumba”

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE