Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya ameitaka wizara inayosimamia wafanyikazi kupitia kwa bodi ya kuajiri wafanyikazi katika kaunti hiyo kuweka mfumo mwafaka utakaosaidia kubaini iwapo watu wanaopewa nafasi hizo wamehitimu au la
Akizungumza afisini mwake katika kikao na walimu wa vyuo vya kiufundi na ECDE kutoka kaunti hii ya Kakamega, Oparanya anasema ipo haja kwa bodi inayowapiga msasa na kukusanya maombi ya kazi kuwa makini wakati wanapokea maombi hayo ili kuepukana na kuajiri wafanyikazi wasiohitimu kutokana na stakabadhi gushi wanasokabidhiwa bila kumakinika.
Gavana huyo aidha ameitaka bodi hiyo kuiga mataifa na kaunti zingine kwa kuweka mfumo ama teknojia maalumu itakayosaidia kubaini iwapo stakabadhi zinazowasilishwa na wanaotuma maombi ya kazi zimefanyiwa ukarabati au la akisema kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza idadi ya wanaopata kazi kwa njia isiyokuwa halali na hivyo kusababisha kupotea kwa mamilioni ya pesa kwa kuwalipa watu wasiohitimu..
Oparanya amesikitikia idadi kubwa ya wafanyikazi wa kaunti hiyo ambao wamekuwa wakipokea mishahara ya bure na hata kuwa vigumu kuwatoa katika orodha wakati wanapogundulikav akidokeza serikali yake haitalaza damu kamwe hadi mbinu mahususi ifuatwe katika kuajiri wafanyikazi wa kaunti hii.
By Lindah Adhiambo