Serikali ya kaunti ya Vihiga inanuia kuwaajiri wahudumu wa afya wa kijamii ambao ni wa kujitolea, katika kile kinachoashiriwa kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika kaunti hiyo.

Akithibitisha hayo, gavana wa kaunti ya Vihiga DKT. Wilber Ottichilo alisema mswada tayari umetayarishwa na kuwasilishwa kwa buge la kaunti hiyo ukisubiri kupitishwa.

Kulingana na gavana huyo, punde tu mswada huo utakapopitishwa, wahudumu hao wa kujitolea wa afya, sasa wataitwa wahudumu wa afya wa jamii.

Gavana Ottichilo amesema hayo akifungua kitengo kipya cha kujifungulia kina mama katika kituo cha afya cha mulele kilichoko katika wadi ya lugaga-wamuluma.

Huku akiwataja wahudumu hao kuwa ni wa umuhimu mkubwa katika ukuaji sekta ya afya, gavana huyo aliahidi kuhakikisha wanapata vifaa bora ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kulingana na gavana Ottichilo, kitengo hicho kitahakikisha kina mama katika eneo hilo wanapokea huduma bora za kuridhisha za kujifungulia.

Alitaja kuwa utawala wake umetoa umuhimu mkubwa kwa sekta ya afya, kwa kupanua miundomsingi, kuwaajiri wafanyikazi zaidi pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa dawa za kutosha.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE