Hatimaye mwili wa mwenda zake aliyekuwa kuhani mkuu wa Kanisa la Kiafrika la Roho Mtakatifu Afrika Mashariki marehemu Shem Daudi Shamala (82yrs), umepumzishwa nyumbani kwake katika kijiji cha Tumbeni katika wadi ya Chemuche eneo bunge la Malava kaunti ya kakamega.

Ni ibaada iliyosimamiwa na katibu mkuu wa kanisa hilo Samson Khalwale iliyoshirikisha madhehebu ya humu nchini na nchi jirani za Uganda na Tanzania.

Hata hivyo kilele cha ibaada hiyo kilishuhudiwa wanasiasa wakijibwaga uwanjani kutumia fursa hiyo na kujipigia debe la uchaguzi mkuu mwaka 2022.

Mbunge wa Malava Malulu Injendi vilevile alitumia nafasi hiyo kwa kupeana rambirambi zake kwa kanisa na jamii huku akijipigia debe kwa maendeleo ameleta kwenye eneo bunge hilo.

Amewataka wanasiasa kupeana heshima wanapohudhuria ibaada ya mazishi na kuwaomba wananchi kuwa waangalifu kwa wale wanasiasa wanaotumia lugha chafu kwenye ibaada za mazishi kwa viongozi wao.

 Wycliffe Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE