Papa Fransisco amewataka wa maaskofu wa kanisa katoliki nchini Marekani kushughulikia msimamo wa rais wa Marekani Joe Biden wa kuunga mkono swala la utoaji mimba kwa njia ya kisiasa badala ya njia ya kitume.
Papa Francis aliyasema hayo alipokua akijibu mjadala wa Maaskofu wa Marekani kuhusu iwapo rais Biden, ambaye ni mkatoliki anapashwa kukataliwa kukomonika au anapaswa kukataliwa kushiriki Ekaristi, kwa maana anaunga mkono haki ya wanawake kuchagua kutoa mimba
Papa Francis alisema utoaji mimba ni “mauaji”, hata muda mfupi baada ya kupata ujauzito. Aliyasema hayo Akiwa amebiri ndege alipokuwa safarini kutoka nchini Slovakia siku ya Jumatano Jumatano.