Chama cha maaskofu kimetilia mkazo usemi wa wanasiasa kutoendesha siasa zao katika kanisa  katoliki na wanatoa wito kwa maafisa wa usalama kuwakamata na kuwafungulia mashtaka viongozi wanao kiuka kanuni za kudhibiti msambao wa covid 19

Chama cha maaskofu wa kanisa katoliku nchini Kenya wakizungumza na wanahabari siku ya Jumatano asubuhi kimehusisha mashambulizi yanayo fanyika kaunti ya Laikipia na sehemu zingine za nchi ikiwa pamoja na Garissa, Marsabit na baadhi ya sehemu za bonde la ufa yanatokana na uchochezi wa kisiasa.

Maaskofu wameitaka serikali kuwapa fidia wakaazi walio adhirika kaunti ya Laikipia na kuwaongeza maafisa wa usalama katika kaunti hiyo ili kulinda Amani.

Aidha maaskofu hao wameahidi kuandaa mazungumzo ya maridhiano baina ya rais na naibu wake huku wakiwataka rais na naibu wake kutoshambuliana kwa maneno hadharani

Wametoa wito kwa serikali kusahau mchakato wa BBI na badala yake kujihusisha na uchaguzi mkuu ujao
By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE