mwili wa mmoja ya walioaga kufuatia ajali ya barabarani, Luyeshe

Mtu mmoja amefariki papo hapo huku mwingine akijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya malava baada ya baiskeli Waliokuwa wameabiri kugongwa na matatu katika eneo la Luyeshe kwenye barabara kuu ya Kakamega–webuye siku ya jumapili jioni.Inadaiwa kuwa matatu hiyo iliyokuwa ikiendeshwa Kwa Kasi ikielekea Kakamega iliwagonga wawili hao Kwa nyuma kabla ya kutoweka.Hata hivyo wenyeji wa soko la Luyeshe wameitaka idara husika ya barabara hiyo kuweka matuta eneo hilo ili kuzuia visa vya ajali vya mara Kwa mara.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE