Wakaazi wa kijiji cha Ivakale katika wadi ya Isukha Kaskazini eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega, wamepigwa na butwaa baada ya kina mama ambao walikuwa wameenda shambani kupalilia miwa kukutana na mwili wa mwanaume mmoja ukiwa umelala kwenye shamba hilo la miwa.
Leo asubuhi tumekuja kwa shamba kupalilia miwa na tumeona mtu amelala kukaribia tukapata ni mwanaume ameshakufa na hapo tukachukua hatua ya kuripoti kwa chief walisema akina mama
Naibu chifu wa Ivakale Joshua Likabo ameelezea kwamba mwanaume huyo anaonekana kunywa dawa ya Actelic Super iliyopatikana kando yake.
Nimearifiwa kwamba kuna mtu amepatikana amekufa ndani ya shamba la miwa na nmekuja nikapata ni kweli. Mtu huyu anaonekana kunywa dawa ya maindi ambayo ni ya Actelic Super maanake tumeipata kando yake alisemanaibu chifu
Anawaomba wananchi kuwacha kujimaliza na kuwahimiza kutembea kila mara na kitambulisho cha kitaifa.
Ukiwa na Tatizo lolote tembelea kituo cha afya uweze kusaidiwa na washauri wanao hudumia wagojwa wa msongo wa mawazo. Na wewe kama mwananchi ukitoka nyumbani tembea na kitambulisha ndo kukitokea na jambo inakua raisi kujua wewe ni nani na unatokea maeneo gani alisema naibu chifu
By Wycliffe Sajida