Majambazi waliokuwa wamejihami na panga na shoka wamemuua mlinzi wa baa moja katik soko la Tangakona/Nambale  na kuiba mali ya thamani isiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Mwenye baa hiyo Charles Kaunda Atelu anasema wezi hao ambao idadi yao haijulikani walimpiga na kumuua mlinzi huyo saa nane usiku kabla ya kuiba pombe, vifaa za muziki na televisheni na kutoweka.
Awali wahalifu walijaribu kuvunja nyumba yake katika eneo la Obekai bila mafanikio jinsi anavyosimulia mkewe.

Kwanza wezi walianza kuvamia nyumba yangu lakini hawakufanikiwa na sasa wamefanikiwa kuvunja nyumba yangu ya biashara na kutoweka na mali ya dhamana na hapo najua ni watu wanajulikana tu na najua pia wamekuwa wakitupigia timing

Kaunda ameungana na wakazi wa soko hilo na mwakilishi wa wadi ya Amukura ya kati Moses Ouma kuwaomba maafisa wa polisi kuzidisha juhudi za kuwakamata majambazi hao ambao wameendeleza visa vya wizi na mauaji katika maeneo mbali mbali ya kaunti ndogo ya Nambale katika siku za hivi karibuni.


Kamishena wa kaunti ndogo ya Nambale anasema polisi wanaendeleza uchunguzi huku pia akiwataka wananchi kusaidia kwa utoa habari wanayofahamu kuhusu visa hivyo.
By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE