Chama cha walimu wa shule za sekondari na vyuo nchini Kenya KUPPET kimeikosa wizara ya michezo kwa kushindwa kufanaya uhamasishaji wa wadau kabla ya utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu wa CBC.
Akizungumza hivi leo KUPPET Akelo Misori amesema hakuna kampeini ya kupinga mtaala huo,ila wizara ya elimu na tume ya kuwaajiri walimu TSC , haijawahamasisha wadau kikamilifu .
Mtaala mpya wa elimu wa CBC ulioanza kutekelezwa miaka minne iliyopita , unaopendekeza wanafunzi kusoma shule ya msingi kwa miaka miwili katika shule ya chekechea ,miaka 6 katika shule ya msingi ,miaka mitatu katika shule ya sekondari na miaka mitatu katika chuo kikuu( 2-6-3-3) .
By Wycliffe Andabwa