Taharuki imetanda katika eneo la Konate kaunti ya Nyamira baada ya mwili wa mwanaume aliyekuwa amekatwakatwa  na kuwekwa kwenye gunia kutupwa kutoka kwa gari lililo kuwa linaenda kwa kasi mida ya saa nane usiku wa jumatatu.

Mashaidi wanaeleza kwamba mwili huo haukua na kijwa na gari lililo tumika halikua na nambari ya usajili

Ripoti ya polisi inaeleza kuwa gunia ilikua na mifuko ya plastiki iliyokuwa imewekwa viungo tofauti vya mwili mzima ila kichwa kikakosekana.

Mwili huo ulipelekwa katika chumba cha kuifadhi wafu cha hospitali ya rufaa ya kaunti ya ya Nyamira na uchunguzi unafanywa kupata chanzo cha mauwaji hayo na waalifu hao

Kamishina wa kaunti ya Nyamira Amos Mariba kupitia kwa kurasa zake za mitandao ya kijamii anasema kwamba mafisa wa DCI washaanza uchunguzi wao . Ameahidi wakaazi wa Nyamira uchunguzi wa haraka na kuwanasa washukiwa  

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE