Daktari aliyeaga baada ya kubugia pombe aina ya Changaa katika kijiji cha Kisia, eneo bunge la Shinyalu amezikwa hii leo, jamii ikitaka uongozi wa mashinani eneo hilo kubadilishwa kwa kuzembea kazini.

Daktari Josphat Kisia alipatikana akiwa hali mahututi na mkewe baada ya kubugia pombe aina ya changaa na juhudi zake kuyaokoa maisha yake zikaambulia patupu.

Wazazi wa mwendazake ambao ni viongozi wa kanisa la baptist nchini  wameguzwa sana na kifo cha ghafla cha mwanao na wanataka suluhu la haraka kwa tatizo la pombe haramu kutafutwa.

Jamii imeulaumu uongozi wa eneo hilo kwa kulifumbia jicho tatizo la madawa ua kulevya yaliyochangia vifo vya wanakijiji na pia kutishia sekta ya elimu eneo hilo.

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE