Serikali ya kitaifa ikishirikiana na ya kaunti imetakiwa kuhakikisha kuwa shilingi bilioni 3 zilizotolewa na rais Uhuru Kenyatta kusaidia wakulima nchini zimewafikia wakulima kaunti ya Bungoma
Mwanasiasa kutoka kaunti ya Bungoma Emmanuel Masuud amesema kuwa mwaka mmoja tangu kutolewa kwa pesa hizo hakuna mkulima hata mmoja kaunti hiyo aliyenufaika na pesa hizo huku wengi wao wakipitia wakati mgumu haswa msimu wa mavuno
Masuud ameitaka serikali kupiga jeki kilimo cha kahawa eneo hilo ili kuwawezesha wakulima kujiinua kimaisha
By James Nadwa