Katika kikundi hiki mwenyekiti wa Lubao Pastors Association amewataka wahisani kujitokeza ili kuwasaidia katika kufanikisha baadhi ya miradi yao walioanzisha na wana upungufu wa fedha.akizungumza katika mkutano uliowaleta pamoja wachungaji wa chama hiki katika eneo la Lubao kaunti ndogo ya Shinyalu kaunti ya Kakamega mwenyekiti wa chama hiki Ibrahim Ambani ameelezea umuhimu wa kukutana kwao .

Mwenye kiti huyo vilevile amewataka wahisani kuingililia kati ili kuwasaidia katika kuwezesha baadhi ya miradi yao kama vile mpango wa kusomesha watoto na pia ule wakununua viti pamoja na hema ambazo mpaka sasa hazijakamilika huku akiwalenga viongozi katika kaunti

Naye katibu wa muungano huu Philip Juma kwa upande wake ametoa  mpangilio kamili kwa wale ambao wangependa kujiunga na kikundi hiki ili kuzuia kutosalia nyuma katika miradi kwa wanao jiunga katika kikundi hiki

Aidha naye mchungaji Joseph Jela amewasifia wenzake kwa kuwajibika haswa mmoja wao anapopatwa na shida kwa kutoa mchango wa kuwafariji

Kwa upande wake Carolyne Lirumbi ambaye ni mweka hazina amesifia kituo cha miamoja na mbili nukta mbili kwa kufanikisha muungano wao huu wa wachungaji na pia kuwataka wanachama kufika mapema ili kuzuia kulipa fini na pia kusifia faida anazopata kama mama

By Mary owano

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE