Wakulima wa pamba katika maeneo ya teso kusini na kaskazini kwenye kaunti ya busia wameibua wasi wasi kuhusu hali ya serikali ya kitaifa na ile ya kaunti kukosa kuwapa mbegu wanazohitaji ili kufufua kiwanda cha kuchambulia pamba cha Balaba-Malakisi.

Wakulima hao wakiongozwa na Aggrey Emojong, wanalalama kwamba tangu kufufuliwa kwa kilimo cha pamba, hakujakuwa na juhudi zozote za kutoa mbegu zifaazo kwa wakulima jambo linalosababisha baadhi yao kununua mbegu kutoka taifa moja jirani, huku wengine wakiamua kukuza mazao ya chakula.

Meneja wa chama cha ushirika cha wakulima cha Jairos, Edward Oteba, ambaye alihutubia waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho alisema kwamba shilingi milioni 8 za ruzuku iliyokusudiwa kukifufua chama hicho zinapaswa kutolewa kwa wakulima.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE