Wanafunzi wawili wa shule ya msingi wamefikishwa mahakamani siku ya Jumatatu, kwa madai ya kufika shuleni wakiwa walevi na kuvuruga amani shuleni humo.

Wanafunzi hao wa shule ya msingi ya Chepkoilel, wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Sango kaunti ndogo ya Saboti baada ya kutiwa mbaroni wakiwa shuleni.

Kamishna wa kaunti ya Trans Nzoia Sammy Ojwang, alisema wasimamizi wa shule hiyo waliripoti kisa hicho kwa chifu wa sehemu ya Kinyoro, Rose Chebet ambaye alifika kwenye shule hiyo akiandamana na maafisa wa polisi waliowatia nguvuni wanafunzi hao.Wawili hao pamoja na wengine kadha wa darasa la sita na saba walitoweka kuepuka kutiwa nguvuni na makachero hao.

Wawili hao waliwaelekeza polisi hadi eneo moja la uuzaji chang’aa mita 600 kutoka shule hiyo ambapo mwanamke mmoja anayeshukiwa kuwa mgema alikamatwa na anahojiwa na maafisa wa polisi.

Wakati wa msako huo polisi walinasa misokoto 400 ya bangi na lita kadha za pombe haramu ya chang’aa. Polisi wamezindua msako mkali dhidi ya uuzaji wa pombe haramu katika sehemu hiyo.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE