Washukiwa watatu wa wizi wa mifugo walikamatwa na kisha ngombe kumi na tatu kupatikana katika kijiji cha Emarba katika eneo la Kajiado ya kati, huku visa vya wizi wa mifugo vikiongezeka katika kaunti ya kajiado.

Duru zinaarifu kuwa  washukiwa hao walikuwa wameiba ngombe 20 kutoka kwa mfugaji mmoja katika kijiji cha  Malili katika kaunti ya Machakos juma lililopita, kabla ya kuzisafirisha hadi kijiji cha Emarba ili kuwauza.

Wazee wa kijiji walifahamishwa na wakaazi, na kisha kuwaarifu maafisa wa usalama ambao walivamia makaazi ya washukiwa na kufanikiwa kuwapata ngombe 13

Inaaminika kuwa washukiwa hao ni miongoni mwa kundi ambalo limekuwa likiwahangaisha wakaazi wa kaunti hiyo na kuwaibia zaidi ya mifugo elfu moja katika muda wa miezi sita iliyopita.

Maafisa wa usalama katika eneo hilo wamebuni mikakati thabiti ya kukabiliana na wizi wa mifugo katika kaunti jirani.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE