Baadhi ya wakazi wa eneo la Ol Moran katika kaunti ya Laikipia wametoroka makazi yao kufuatia visa kadhaa vya mashambulizi ya majambazi.

Haya yanajiri huku baraza la kitaifa la ushauri kuhusu maswala ya kiusalama likikutana leo kushauriana kuhusu hali ya utovu wa usalama katika kaunti hiyo.

Watu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi huku mvulana wa darasa la nane akijeruhiwa vibaya na wezi wa mifugo siku ya ijumaa. Msichana wa umri wa miaka 12 pia anauguza majeraha ya risasi katika hospitali ya kujifungulia kina mama ya sipili baada ya kupigwa risasi na majambazi muda mfupi baada ya saa moja usiku alipokuwa akichota maji.

Mshirikishi wa eneo la Rift Valley George Natembeya alitoa wito wa utulivu na kuwahimiza wakazi kurejea kwenye makazi yao akiwahakikishia kwamba serikali imeimarisha usalama kwenye eneo hilo.

Mbunge wa Laikipia kaskazini Sarah Korere, na viongozi wengine wa aeneo hilo walishtumu maafisa wakuu wa usalama katika kaunti hiyo kwa kupuuza taarifa za kijasusi zilizotolewa na viongozi kuhusu uwezekano wa kutekelezwa kwa mashambulizi.

Wakati huo huo gavana wa Laikipia Nderitu Muriithi alitoa onyo kali dhidi ya majambazi wanaowahangaisha wakazi wa Ol Moran, Sossian na Githiga kuwa chuma chao ki motoni.

Gavana huyo alisema serikali yake inafanya kila iwezalo kuhakikisha majangili hao wanakibiliwa kisheria.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE