Leo ikiwa ni tarehe kumi mwezi wa sita  mwaka wa eifu mbili ishirini na moja, wanahabari wa lubao walienda kuzuru msitu wa Kakamega. njiani, tuliliona Kanisa la Kikatoliki la Lubao na pia kuona Gereza la wafugwa la wanaume la Shikusa.

katika pitapita zetu kwenye msitu wa Kakamega almaarufu kama Kakamega Forest,tulikutana na mzee wa kijiji cha Shilongo ambaye anatambulika kwa jina la Ernest Ikutwa Shivisi. kijiji chake kimepakana sako kwa bako na msitu wa Kakamega .bwana Ernest alituambia mambo kadha wa kadha kuhusu msitu wa  Kakamega.

Bwana Ernest alitueliza kuwa msitu huu umeweza kuwafaidi wanakijiji kwa njia  kadha wa kadha.kupitia msitu huo,wanakijiji wameweza kupata mahali pa kuwalisha mifugo wao almradi tu wamekata risiti. kukata risiti kunawazuia kukamatwa na polisi wakati wanawalisha mifugo wao.

Bwana Ernest alisema kuwa wale wanaokaidi kukata risiti hujiweka katika hatari  ya kukamatwa na maafisa wa KWF.bwana Ernest alisema kuwaili mtu kuwajua mifugo wake, wao huskiza milio ya ya kengele kwani milio hiyo hutofautiana kutoka kwa ngombe mmoja hadi mwingine.

Ernest aliendelea kusema kuwa kwa usalama wa wanakijiji wa sehemu ya lilongo wao hushauriwa kutembea na wembe kwani ndani ya msitu huo kuna aina ya nyoka wanao aminika kuwa wakali kabisa  Africa nzima.hii inawalazimu wanakijiji kutembea na wembe ndiposa  wanapovamiwa na nhoka hawa ambao wanaaminika kuwa hatari,basi wanakata mahali walipovamiwa ili kuzuia kusambaa kwa sumu hiyo hatari mwilini.

Bwana Ernest  alimaliza kwa kutuambia kuwa hapo ndani kuna aina tofauti tofauti ya viwanja ambavyo vimepewa majina kulingana na aina ya miti iliyo izingira na mwishowe kusema kuwa angependa serikali  iwafwatilie na kuwakamata wanaoharibu miti na si kuwalaumu wanakijiji kwa kuharibu miti kwani msitu huo hutumika na wengi.

Baadaye tulirudi kwenye afisi tukiwa na na mwanga kuhusu msitu wa Kakamega.

By Mary Owano

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE