Takribani maskwota 1,500 kutoka kaunti ndogo za Lugari na Likuyani ambao ni wahasiriwa wa vita vya kikabila mwaka 1992 wameunga mkono hatua ya mbunge wa Likuyani daktari Enoch Kibunguchy kupinga mipango ya mamlaka ya mazingira nchini NEMA kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Kakamega kutaka kutwaa zaidi ya hekari 460 za ardhi kwenyei msitu wa Turbo kwa ajili ya shughuli za kilimo chini ya serikali ya kaunti.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Jotham Wanjala wamesema ingekuwa vyema kwa serikali kuwapa mashamba kwenye msitu huo walivyoahidiwa  kabla ya kutekeleza mpango huo wa kilimo.

Mbunge wa eneo hilo dr. Enoch Kibunguchy ameapa kupinga mpango huo akihoji kuwepo njama ya baadhi ya viongozi katika serikali ya kaunti ya Kakamega kutaka kujinufaisha na ardhi hiyo.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE