Waziri wa ardhi  miundo misingi na mali asili katika kaunti ya Kamamega Robert Kundu Makhanu ametoa ilani kali kwa wakazi ambao wamenyakuwa vipande vya ardhi vya serikali katika kaunti hiyo  kuvirejesha kwa hiyari pasi na kishinikizwa na serikali.

Akizungumza baada ya kurejesha shamba hekari kumi ambalo lilikuwa limenyakuliwa na wakazi katika kidimbwi cha kimani mtaa  wa Lusweti eneo bunge la Likuyani ,Makhanu alihoji kuwa serikali ya kaunti ya Kakamega imeanzisha mikakati ya kurejesha vipande vyote vya ardhi ambavyo vimenyakuliwa katika kaunti hiyo.

Aidha Makhanu ametoa ilani kali kwa wakazi ambao wamenyakuwa vipande vya ardhi vya serikali katika kaunti ya Kakamega, kurejesha kwa hiyari pasi na kushikizwa na serikali.

Mbali na hayo Makhanu ameelezea kuwa serikali hiyo ina mpango wa kufungua ofisi za kushughulikia hati miliki za mashamba , na kufungua mahakama katika eneo na Likuyani ili kurahizisha hudumu hizo muhimu kwa wananchi wa kaunti hiyo.

Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE