Ipo njama ya kusambaratisha chama cha F-Kenya ili kisiwe na nguvu ya kuzoa viti vyote katika kaunti ya bungoma kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Ni madai ya Collins Wakoli ambaye anasimamia maswala ya vijana katika chama hicho,kwenye taarifa kwa wana habari wakoli amedai kuwa malumbano ya mara kwa mara katika uongozi wa chama hicho yanatokana na msukumo wa nje.

Wakoli aidha ametoa ushauri kwa bodi kuu ya chama hicho[KNECK] kuingilia kati ili kukinusuru chama hicho ambacho amedai kuwa kiko katika nafasi bora ya kutwaa uongozi  na nyadhfa zinginezo mingi itimiyapo mwaka wa elfu mbili na ishirini na mbili.

Wakati uo huo wakoli amewashauri viongozi haswaa wa ukanda huu wa magharibi kuongea kwa sauti moja kama mojawapo ya njia ya kuyavutia kabila zingine kuunga mmoja wao mkono.

Hivi maajuzi kumeshuhudiwa mirengo zaidi ya tatu katika chama cha f-kenya swala ambalo limesababisha migwaruzano si haba.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE