Kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa KNUT Wilson Sosion siku moja kabla ya uchaguzi wa kitaifa wa muungano huo kulichochewa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi serikalini.
Kwa mujibu wa Katibu wa KNUT Tawi la Bungoma Mshariki Aggrey Namisi, Sosion alishinikizwa kujiuzulu kwa madai kuwa angekuwa tishio la usalama endapo angeshiriki uchaguzi huo.
Wakati ou huo, Namisi amemuomba Sosion kushirikiana na uongozi mpya wa KNUT chini ya Katibu Mkuu mpya Collins Oyuu ili kufanikisha haki za walimu chini ya mwavuli huo wa KNUT.
By Hillary Karungani