Wachuzi katika soko la Kakamega wamelalamikia kuangaishwa na vijana wa kurandaranda kwa kuwarushia vitoa machozi kupelekea mmoja wa kike kulazwa katika hospitali kuu ya Kakamega akivuja damu kutoka tumboni.
Wachuzi hao hasa kina mama wa kuuza mboga, mahindi makaa na nguo wanadai kutishiwa maisha na vijana hao maarufu kama chokora, ambao wameongezeko kupindukia, huku wakiwarushia vitoa machozi wakipendekeza mirundiko za taka kuondolewa ambazo zinaonekana kuwavutia wahusika.
Wanadai siku chache zilizopita walijeruhi mmoja wa mama ambaye hadi wa sasa amelazwa katika hospitali kuu ya Kakamega akivuja damu, wakitaka serikali ya kaunti hiyo kuwaondoa vijana husika katikati mwa mji huo kwani wamebadili na kuwa wahalifu.
Aidha vijana wamesema wao uokota mikope ya kutoa machozi kwenye takataka, wakipinga hatua ya wao kuondolewa sawa na kuondoa mirundiko ya taka kwa kile wanachodai ndio kitega uchumi kwa wao.
By Sajida Javan