Muungano wa wafanyikazi kaunti ya Kakamega umejitokeza na kushtumu tume ya kutathmin mishahara  SRC kuondoa nyongeza ya mishahara kwa wafanyikazi wa umma.

Mwenyekiti wa muungano huo Allan Nambemba, anasema ni jambo la kushangaza kwa tume hiyo kuchukua uamuzi huo ikizingatiwa miaka nenda rudi wafanyikazi wa umma wamekuwa wakipitia hali ngumu ya maisha kwa kukosa nyongesa ya miashahara.

Aidha muungano huo umenyoshea lawama waziri wa afya Mtai Kagwe kufuatia kusambaa kwa kasi ugonjwa wa korona, licha ya kuruhusu sherehe za Madaraka kuandaliwa jijini Kisumu, baada ya serikali kutangaza aina mpya ya janga hilo katika eneo la Kisumu.

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE