Napoli wameamua kumfanya mlinzi wa Arsenal Mskochi Kieran Tierney lengo lao la muda mrefu baada ya kumkosa nyota huyo aliye na umri wa miaka 23 mwanzo wa msimu huu.

Hayo yakijiri klabu ya Manchester United inajiandaa kumenyana na Paris St-Germain katika mbio za kumsaka kiungo wa kati wa Brest na Ufaransa mwenye chini ya miaka 21

Huku Klabu ya Everton wanatafakari uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati Mbrazil Felipe Anderson, 27, ambaye yuko Porto kwa mkopo kutoka West Ham United.

Na klabu ya Chelsea hawako tayari kumuachilia kiungo wa kati wa England Ross Barkley kujiunga na Aston Villa – ambako anacheza kwa mkopo wa msimu mzima -huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akisalia na miaka miwili na nusu kwenye mkataba wake.

Story by Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE