Madereva wa taxi mjini eldoret wametoa malalamishi kwa serikali ya kaunti kwa kuwafurusha mahali pa biashara na kisha kuchukua magari yao.

Madereva hao wamepata magari yao yamechukuliwa licha ya kulipa kodi ya elfu mbili na mia tano kila mwezi kisha kuwafurusha na kukosa kuambiwa mahali wanafaa kuendeleza biashara yao.

Hata hivyo madereva hao wanadai kuwa hawakupewa ilani ya kuhama mahali pale vile vile wametoa wito kwa gavana wa kaunti Jackson Mandago kuingilia kati na kuwasaidia.

Wakati huo huo wakili Kimani Wanjohi amesihi kuwa wamepea serikali ya kaunti onyo ya muda ya wiki moja ili watafute suluhu ya kudumu ama wachukuwe hatua kwa kupeleka suala hilo kortini.

Story By Sharon Lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE