Viongozi wa chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT tawi la Busia wameelezea matumaini ya kuimarisha chama hicho kwa kufanya majadiliano na Tume ya huduma za walimu TSC baada ya kukamilisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Mwenyekiti wa KNUT tawi la Busia Justin Majale amesema kwamba wanalenga kufanya mazungumzo na serikali pamoja na TSC kuhakikisha chama hicho kinaimarika na kuendelea kunufaisha walimu.
Haya yanajiri huku kukiwepo mvutano kati ya TSC na KNUT, chama hicho kikilaumu TSC kwa msingi kuwa imechangia masaibu yanayokikumba ikiwemo kuwadhulumu wanachama wake, kukosa ufadhili na hata wanachama wake kuondoka na kujiunga na vyama vingine ikiwemo KUPPET
KNUT sasa ina wanachama wasiozidi elfu ishirini na nane kote nchini ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka ya hapo awali ambapo KNUT kilikuwa na wanachama zaidi ya laki mbili kote nchini.
Story by Hillary Karungani