Shughuli za uchukuzi zimetatizika kwa muda kwenye barabara ya Muyayi kuelekea Ndengelwa katika wadi ya Bukembe Magharibi kaunti ya Bungoma baada ya wahudumu wa bodaboda wakishirikiana na wakazi kuandaa maandamano na hata kupanda migomba ya ndizi kwenye barabara hiyo wakimlaumu mwakilishi wa wadi ya Bukembe Magharibi Anthony Lusenaka kwa kile wanachodai ni kuhadaiwa kwa kipindi kirefu bila kuikarabati barabara hiyo.

Hali mbaya ya barabara hiyo imeathiri pakubwa shughuli za uchukuzi huku baadhi ya wagonjwa hasa akina mamawajawazito wakilazimika kujifungua wakiwa barabarani kwa kushindwa kufika hospitalini.

Wakazi hao aidha wameibua madai ya kutishiwa kila mara wanapotoa kilio chao kuhusu barabara hiyo wakimlaumu mwakilishi wadi wa eneo hilo Anthony Lusenaka kwa kushirikiana na Polisi kuwadhulumu wakazi.

Story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE