Hatimaye wagombeaji 15 akiwemo mama mmoja wameidhinishwa rasmi kugombea kiti cha ubunge cha Matungu kwenye uchaguzi mdogo wa tarehe nne mwesi Machi.

Wa mwisho kuidhinishwa ni aliyekuwa mbunge wa zamani David Were wa chama cha ODM ambaye baada ya kuidhinishwa na tume ya uchaguzi na mipaka IEBC amewataka wenyeji wa  Matungu kumpigia Kura kuendeleza miradi ambazo alikuwa ameanzisha.

Kwa upande wake gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya ambaye pia ni Naibu kinara wa chama cha ODM aliongoza viongozi wengine akiwemo seneta wa Siaya Jemes otengo na mbunge wa suna Junet Mohammed wamesema kuwa Were ana ujuzi hitajika kuwakilisha wengine wa Matungu kwani ana uzoefu wa kuwa bungeni ukilinganisha na waniaji wengine.

Wakati huo uo msimamizi wa uchaguzi eneo hilo John kirui akiwataka waniaji hao kufanya Kwa Amani wakizingitia masharti ya uchaguzi.

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE