By Dorothy Iraya
Mchuuzi mmoja wa ng’ombe katika soko la Jebrock ameuawa kufuatia ugomvi uliodaiwa kusababishwa na deni la shilingi elfu moja kati yake na mwenzake wa biashara hiyo. Tukio hilo limezua hofu miongoni mwa wafanyabiashara katika eneo hilo huku polisi wakiendelea na uchunguzi kamili.

Ni tukio lililowaacha wachuuzi na wafanyabiashara katika hali ya mshangao na huzuni, baada ya mchuuzi huyo kuaga alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ndogo ya Pona Health Centre Jebrock, kufuatia mzozo ulioibuka kati yake na mchuuzi mwenzake, kufuatia deni la shilingi elfu moja.Nancy Ilamwenya ni aliyeshuhudia tukio hilo.
Familia ya marehemu imetaka haki itendeke huku ikieleza kusikitishwa na namna maisha ya mpendwa wao yalivyokatizwa kwa sababu ya fedha kidogo, huku ikiiomba serikali na idara ya upelelezi kaunti ya Vihiga kufanya uchunguzi wake na kuitendea haki familia yao.

Chifu wa lokesheni ya Jepkoyai Peter Keya amewarai wenye familia kuwa watulivu na kungoja haki itendeke huku akiwaomba wafanyabiashara wa soko ka Jebrock kutochukua sheria mikononi wakati kunakuwa na mizozo ya aina hii..