Mihadarati imetajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya Visa vya utovi wa nidhamu mwambao wa pwani hasa eneo la Likoni kwani vijana wengi wameingilia utumizi wa dawa za kulevya na kuwa waraibu huku wakijiingiza katika vitendo visivyo vya kawaida kupata pesa za kununua dawa hizo.
Haya ni Kulingana na Mbunge wa Likoni Mishi Mboko ambaye ametoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuingilia Kati na kunusuru hali hiyo kwa kuwashika na kuwafungulia mashtaka wale wanaohusika na biashara hizo za dawa za kulevya pwani.
Story by Alovi Joseph