Wakenya wengi wanazidi kutoa hisia zao mtandaoni kuhusu ni kwa nini ujumbe wa heri njema wa Rais Uhuru Kenyatta kwa mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwenye mtandao rasmi wa ikulu ya Rais umefutwa.

Kwenye ujumbe huo, Rais alimpongeza Museveni kwa kuibuka mshindi kuongoza taifa hilo  kwa hatamu ya sita Kulingana na matokeo yaliyotangazwa na tume ya Uchaguzi nchini humo kufuatia uchaguzi mkuu ulioandaliwa tarehe 14 mwezi huu.

Hata hivyo, baada ya maoni ya watumizi ya mtandao, ujumbe huo ulifutwa baada ya Rais kukejelewa ni kwa nini apongeze Museveni ilhali uchaguzi wenyewe ulidaiwa kukumbwa na dosari kuashiria ukoloni mamboleo.

Huku hayo yakijiri, mpinzani wake wa Karbu Museveni ambaye alikuwa mwanamziki na kugeuka kuwa mwanasiasa, Bob Wine, kwa sasa amezuiliwa nyumbani kwake na amelalamikia hatua hiyo ya yeye kunyimwa haki ya kimsingi ya kutangamana na watu.

Kupitia kwa mahojiano na shirika la habari la BBC, Bob Wine amelalamikia swala la ukosefu wa chakula na mahitaji mengine huku familia yake akiwemo mkewe kudhulumiwa na maafisa wa polisi.

Story by Alovi Joseph

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE