Mlinzi wa kulia wa Atletico Madrid Kieran Trippier,wa miaka 30, amewaambia wachezaji wenzake wa England yuko na mpango wa kujiunga na Manchester United msimu huu
Hayo yakijiri Barcelona wanafikiria kutoa ofa iliyoboreshwa kwa kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum mwenye umri wa miaka 30 ambaye anajiandaa kuondoka Liverpool kwa uhamisho huru, baada ya Paris St-Germain kupoteza ofa ya awali ya Barca
Ikiwa Barcelona haitakamilisha usajili wa Wijnaldum na Memphis Depay mwenye umri wa miaka 27 wa Uholanzi kutoka Lyon wiki ijayo inaweza kuwauza hadi wachezaji wanne kwa ujumla
By Samson Nyongesa