Viongozi wa wakulima wa miwa kutoka eneo la Mumias sasa wanamtaka mweekezaji yeyote mwenye nia ya kufufua kiwanda cha Mumias kuwahusisha wakulima moja kwa moja na pasipo kuwategemea wanasiasa ambao hawana nia njema na ufufuzi wa kiwanda hicho
wakiongozwa na mwakilishi wadi wa East Wanga Shabaan Otengo wamewasuta baadhi ya wanasiasa kwa kuwa kizingiti katika juhudi za kufufua Mumias
Otengo amesema itakuwa vyema mwekezaji kuja moja kwa moja kuongea na wakulima
Mwakilishi huyo aidha ameitaka serikali ya kitaifa kujitokeza waziwazi na kueleza mpango wa kuwasaidia wakulima katika ufufuzi wa kiwanda cha Mumias
By Lindah Adhiambo